Tuesday, October 1, 2013

KUSHUKA KWA UFAULU WA WANAFUNZI DARASA LA SABA-2012

UNAFAHAMU NINI...... WIKI ILIYOITA TULIONA KUWA KUNA SABABU KUU TANO(5) AMBAZO ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI : KUNA ZILE ZINAZOMUHUSU:
  1.  MZAZI
  2. MWANAFUNZI
  3. MWALIMU
  4. SERIKALI
  5. LUGHA YA KUFUNDISHIA
WIKI ILIYOPITA TULIANGALIA UPANDE WA MZAZI, LEO TUTAANGALIA UPANDE WA MWANAFUNZI;
  •  Mwanafunzi si kwamba anapoingia darasani hana chochote kichwani hapana bali ili uwezo na maarifa aliyonayo aweze kuyatoa kinahitajika kiunganishi kiitwacho LUGHA Kama hakuna lugha anayoielewa yeye na yule anayemfundisha wakaelewana basi hata utumia mitambo na mbinu yoyote ile huwezi kumwelekeza mwanafunzi akaelewa na yeye akajieleza na kutoa aliyonayo.Kwa maana nyingine kitaalam tunasema hapo hakuna "TENDO LA KUJIFUNZA"
  • Ushauri kwa wanaohusika na wadau wote wa elimu kwa ujumla kuchukua uamuzi mgumu ~ KUJIPANGA NA KUBADILI LUGHA YA KUFUNDISHIA SHULE ZA MSINGI ILI IENDANE NA ILE YA SHULE ZA MSINGI-YAANI "KIINGEREZA"
                                          ....Ni ushauri tu.......Mwl.Mzoefu darasani...!!!