Tuesday, October 7, 2014

MWALIMU NA UALIMU!!

KUWA MWALIMU SI KAZI BALI UALIMU NI KAZI NGUMU SANA:-
   Unajua ukichukua jukumu tu la kuwafundisha wenzako tayari utaitwa "Mwalimu" lakini huna cheti rasmi cha kazi hiyo, hivyo ndivyo unavyoweza kuitwa Mwalimu.
   Sasa ualimu sio hivyo unavyodhani.Ualimu ni matendo yote mwalimu anayopaswa kuandaa kabla hajaingia darasani na hayo ndiyo mwalimu huyu anapaswa kuyasomea na kisha kuyafanyia kazi ili kuitendea haki fani hii.
   Hakika ugumu wa kazi hii umekalia pale ambapo kila unapotaka kumpatia mwanafunzi ufahamu wa namna yoyote ile ni lazima ufuate taratibu zote. taratibu hizo ni pamoja na:-
  1. Kuandaa somo
  2. Kuandaa maelezo mafupi (Notes)
  3. Kuandaa zana za kufundishia
  4. Kuingia darasani na kuanza kufuatilia ufundishaji kama ulivyoandaa - yaani kwa kufuata kipengele kwa kipengele muda kwa muda na mwisho kumpatia kazi ya kufanya mwanafunzi na kusahihisha kazi yake
  5. Kazi za kufanya baada ya kutoka darasani ni pamoja na;-
  • Kumalizia kusahihisha
  • Kuandika tathmini na maoni
  • Kujaza daftari la uthibitisho kama umefundisha(Class log book)
  • Kujaza daftari la mada uliyofundisha/shajara (Subjects log book) 
Taratibu hizi na zile ambazo sijazitaja zifanywe kwa kila somo unalokwenda kulifundisha siku hiyo-sasa hiyo ni tisa kumi kwa siku mwalimu ana masomo zaidi ya matano kulingana na uchache wa walimu katika shule husika anayopaswa kuyafundisha na kufuata taratibu zote nilizozieleza hapo juu
   Sema sasa, Je, mwalimu unaweza kumwekea kipimo cha ufundishaji wake kwa siku? Hapana, kinachofanyika ni kuwa,mwingine ataonesha bidii na mwingine atategea.! Lakini mwisho wa mwezi mshahara wa mtegaji na mchapa kazi hakuna tofauti!!
USHAURI:
  Kama -"Mwalimu Mzoefu Darasani" nashauri ,ili Mchapakazi asikatishwa tamaa na Mtegaji - Serikali iandae malipo ya ziada (Bonasi) kwa mwalimu anayetimiza majukumu yake barabara mara tu baada ya wakaguzi wa shule kuthibitisha hilo - Kwa utafiti wangu nimegundua wakaguzi wakikagua utasikia wakisema - mwalimu huyu ana asilimia 80 na mwingine asilimia 30 na wanaishia kusifu tu kwa maneno aliyefanya vizuri na kumkemea yule aliyefanya vibaya zoezi huishia hapo. - Hapo mimi sijaona motisha iko wapi....Kwa leo inatosha - siku nyingine Tchao!!
              >>>>>>>Na "Mwalimu Mzoefu Darasani">>>>>>> 
             

MWALIMU NA UALIMU

MWALIMU NA UALIMU

Monday, October 6, 2014

JUMATATU - SIKU YA KAZI

TUKICHAPA KAZI KWA NIA NA MALENGO TUTAONGEZA KIPATO CHETU NA TAIFA KWA UJUMLA.TUCHAPE KAZI KWA MOYO NA UPENDO WA KUWAHUDUMIA WENZETU.


IPENDE KAZI YAKO KWANI HUKULAZIMISHWA KUIFANYA.KUMBUKA KUWA MZALENDO KWA NCHI YAKO KAMA WENZETU ULAYA NA MAREKANI WANAVYOITETEA NCHI YAO KWA HALI NA MALI - TUWE HIVYO SI KILA KUKICHA NI LAWAMA TU ! HEBU TUFANYE KAZI TUONE KAMA HATUTALETA MABADILIKO!!









........Ni ushauri tu ....na Mwalimu Mzoefu Darasani........!!!