Wednesday, March 23, 2016

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUISHI MIAKA MINGI:

UNATAKA KUISHI MIAKA MINGI?....BASI UNALAZIMIKA KUFANYA HAYA:-
1.Kabili msongo wa mawazo:
          Usiwaze sana katika maisha yako ya kila siku jaribu kuridhika na unachokifanya na kukiamini.
2.Ishi maisha chanya/Kucheka:
          Kulalamika kwa!kila jambo unakaribisha maradhi ya moyo..acha!
3.Fanya mazoezi na pata usingizi wa kutosha:
          Uzito mkubwa wa mafuta mengi ni nyumba ya magonjwa ya moyo...fanya mazoezi!!
4.Tabia zako/Ulaji wa yakula:
          Tusipende kuvuta sigara,ulevi, ngono zembe,kula vyakula vya mafuta ya maji maji k.v nyama,tusile wanga kwa wingi.Kwa kufanya hivyo tutakaribisha;Bp,Stroke,Moyo,Kansa,Unene na Kisukari,Tule vyakula vya asili k,m,Mbogamboga,maji mengi,matunda kwa wingi
5.Dini:
          Kujengwa kiroho,kumtumainia Mungu,kuhudhuria katika nyumba za ibada hurefusha maisha.
6.Kunywa maji mengi:
          Maji mengi mwilini husafisha figo na ini na kuondoa uchafu uliomo.
N/B:- Ni matumaini yangu umeambulia kitu kwa siku ya leo,basi siku nyingine fungua Blog hii ya "Mwl Mzoefu Darasani' upate maarifa mapya ya kimaisha, kielimu na kiafya;;;;;Tchao...!! 

                                                                            (MMD)