Saturday, July 19, 2014

UMEFIKA KATIKA KANISA HILI LA HIJA - HAPA MPANDA, KATAVI?

!!....Tembelea siku moja ufanye hija yako hapa kanisa la hija la Ilembo nje kidogo ya mji wa Mpanda.......!!

 !!Ni kanisa la hija lijulikanalo kama - Ilembo
    ~~~~Na Mwl.Mzoefu~~~~

                                                                              !!Wana-kwaya wa Parokia ya Ilembo!!
!! Wanatoka kanisani ibada imekwisha!!

LEO KATIKA AFYA NA MWL.MZOEFU DARASANI!!

>>>>ASALI NA MDALASINI USIKATIKE NYUMBANI KWAKO<<<<<
MAFUA NI UGONJWA UNAOWAKERA WATU WENGI SANA NA KUWANYIMA RAHA.LEO NAKUPATIA KAUJANJA KA NAMNA YA KUIONGOA HALI HII.

  •    CHUKUA KIJIKO KIMOJA CHA ASALI
  •    ROBO KIJIKO CHA MDALASINI KISHA CHANGANYA.
N/B:- TUMIA ASUBUHI ,MCHANA NA JIONI.MAFUA YAKO YATAKWISHA KABISA.
          MUHIMU HAPA NI KUWA NA ASALI WAKATI WOTE KWANI ASALI NI CHAKULA 
          NA DAWA.
               ~~~~~~~~~Ni usahuri wa bure tu na Mwalimu Mzoefu Darasani~~~~~~~~

Wednesday, July 9, 2014

MWALIMU MZOEFU DARASANI- NA UJASILIAMALI

UTAFANYA NINI BAADA YA MAISHA HAYA YA KAZI YA KULIELIMISHA TAIFA?
  • JE,UTAOMBA TENA MKATABA WA KAZI?
  • UTASALIA NYUMBANI TU?
  • UTAANZA KUNUNUA NYUMBA YA KUISHI?
  • UTAKUWA TEGEMEZI KWA WANAO?
  • UTAFANYA BIASHARA?

LEO MIMI NAKUSHAURI UANZA KUJIFUNZA "BIASHARA" ILI IANZA KUKUZOEA KABLA HUJASTAAFU MWALIMU WANGU!!
      BIASHARA SI MTAJI PEKEE BALI NI "KUTHUBUTU" BASI NAKUSII ANZA LEO KUTHUBUTU KABLA HATA HUJASTAAFU MUNGU AKIKUJALIA.UTAKAPO KUWA TAYARI NDANI YA BIASHARA ITAKUWA RAHISI KWAKO KUTUMIA KAKIINUA MGONGO KATIKA KUIMARISHA BIASHARA YAKO TU BADALA YA KUSUBIRI MPAKA UNASTAAFU NDIPO UANZA MARA - NYUMBA, BIASHARA MASHAMBA N.K.
      BASI LEO NIKUPATIE VIONJO VYA NAMNA YA KUFANYA BIASHARA ANGALAU NDOGO:-MAMBO 7 YA KUZINGATIA KATIKA BIASHARA:-
     
   

 1.THAMINISHA BIASHARA YAKO:
Iwe biashara kubwa au ndogo kumbuka bidhaa unazouza ni muhimu ziwe zenye ubora na mwonekano mzuri unaovutia wateja.("Good business man serves quality products to his customers")
                                                                                      
    

 2. PATA USHAURI KWA WATU WALIOFANIKIWA KI-BIASHARA:

Unapopata utata katika kufanya maamuzi sahihi ya nama ya kuanza biashara ni vizuri utafute ushauri kutoka kwa watu ambao tayari wamefanikiwa katika biashara kama yako.
    

 3.FANYA BIASHARA YA KIPEKEE:

Kuwa mbunifu katika kubuni na kuibua aina ya biashara
    

 4.UZA BIDHAA KWA BEI INAYOKUBALIKA NA WENGI:

Hapa haina maana uuze kwa bei poa bali uza kwa bei ambayo wengi wanaweza kuimudu.
   

  5.TANGAZA BIASHARA YAKO:

Biashara ni matangazo hivyo huna budi kuitangaza redioni,runinga,magazeti,vipeperushi,mabango n.k.
   

  6.JIAMINI NA USIKATE TAMAA KATIKA BIASHARA:

Kuna wakati na hasa unaponza biashara mambo huwa mabaya na hivyo ukaanza kukata tamaa,ni vyema ukajiamini na kutafakari na kujua ni wapi ulikosea na nini cha kufanya ili uboreshe biashara yako.
    

 7.FANYA BIASHARA UIPENDAYO:

Naamini mtu ukiifanya kazi uipendayo utaifanya kwa uhodari na kupata mafanikio!
                         <<<<<"BIASHARA NI WATU"!!>>>>>
                                                    =====Na Mwalimu Mzoefu Darasani====!!
>> Huu ni ushauri wa bure....kwani mwisho wa maisha yetu ya ualimu tunaujua sisi wenyewe>>....!!

MWALIMU MZOEFU DARASANI- NA UJASILIAMALI

UTAFANYA NINI BAADA YA MAISHA HAYA YA KAZI YA KULIELIMISHA TAIFA?
  • JE,

MWALIMU MZOEFU DARASANI- NA UJASILIAMALI

UTAFANYA NINI BAADA YA MAISHA HAYA YA KAZI YA KULIELIMISHA TAIFA?

MWALIMU MZOEFU DARASANI- NA UJASILIAMALI

MWALIMU MZOEFU DARASANI

MWALIMU MZOEFU DARASANI NA UJASILIAMALI

MWALIMU MZOEFU DARASANI

Saturday, July 5, 2014

DK. 30 - 45 TU ZA MAZOEZI YA VIUNGO KWA SIKU

                    <<>>

1.NI DAWA YA KUEPUKANA NA MAGONJWA YAFUAYO:-
  • PRESSURE
  • MOYO
  • BARIDI
  • KISUKARI
  • SARATANI
  • AKILI
  • UZITO
  • MIFUPA(Osteoporosis)
2.HUREFUSHA MAISHA KWA:-
  • KUWA NA AFYA NJEMA.
  • KUTIBU NA KUEPUKANA NA MAGONJWA MENGI ANAYOWEZA KUEPUKIKA.
  • KUIMARISHA AFYA YAKO.
  • KUIFANYA MIFUMO MBALIMBALI YA MWILI (K.V.MFUMO WA FAHAMU,DAMU,HOMONI,CHAKULA NA MISULI IFANYE KAZI SAWA SAWA.
  • KUUCHANGAMSHA MWILI.
  • KUUFANYA UWE NA KUMBUKUMBU NZURI.
  • KUWA SHUPAVU.
  • KUWA MTU UNAYEJIAMINI.
  • KUREKEBISHA KIWANGO CHA MAFUTA MWILINI.
  • KUPUNGUZA HIGH BLOOD PRESSURE.
  • KUONGEZA HAMU YA KULA.
  • KUPUNGUZA UZITO N.K.
N/B:-
         MWALIMU "MZOEFU DARASANI" LEO NASEMA HIVII...PIGA, UWA, GALAGAZA,CHOCHOTE ULICHOKIPANGA LEO HAKITAFANIKIWA BILA KUWEPO KWA AFYA NJEMA......NAKUSIHI ILI KUWA MTU WA KISASA MWALIMU WA KISASA,MSOMI NA MWENYE TAALUMA INAYOWEZA KUTUMIKA NA KUTUMIWA NA WENGINE,>>>FANYA MAZOEZI KWA DAKIKA 30 - 45 KWA SIKU KWA FAIDA YAKO,FAMILIA YAKO NA TAIFA KWA UJUMLA
                   >>>>>>>>>Ni ushauri tu ....Na Mwalimu Mzoefu Darasani>>>>>>
>>Uwe mjasiliamali - Mazoezi ni dawa ya kwanza kabla ya dawa za hospitalini...fanya mazoezi ya viungo.
 >>Pamoja na uzuri wako bila afya njema kazi bure...fanya mazoezi mke wangu!!


>>Hata mandhari ya sebule yako utaifurahia uki
                           wa na afya njema.


 >>Fanya mazoezi upate furaha katika maisha
>>Kama unataka kustawi kama maua hayo fanya mazoezi rafiki!

>>Unaliona dume hilo linatakiwa kuondoa kitambi hicho kwa mazoezi!

<
                                 kwa afya mgogoro.


>>Watu wazima ndo kabisaa-magonjwa ni mengi.

<
>Hata rais anatakiwa kuwa 'rais' wa mazoezi ya 
                                                                                          viungo pia kwa faida yake na taifa lake.
<<NI MWL.MZOEFU DARASANI!!>>

Thursday, July 3, 2014

"HEBU ...KAMA WALIMU TUZINGATIE HAYA MAMBO 15 KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU"

"WALIMU NA MAISHA YETU YA KILA SIKU:"
    SISI WALIMU KUTOKANA NA KAZI ZETU TUNAZOZIFANYA AMBAPO TUNAKOSA HATA MUDA WA KUFUATILIA MSTAKABARI WA MAISHA YETU NA FAMILIA ZETU,TUMEKUWA WEPESI SANA WA KUKATA TAMAA YA MAISHA AU KURAHISISHA MAISHA NA KUSALIA MIAKA NENDA MIAKA RUDI - TUKIRIDHIKA NA HALI YA MAISHA YA CHINI.
    MIMI KAMA "MWALIMU MZOEFU DARASANI" NATAKA NIKUPATIE KANUNI ZA MAISHA YETU YA KILA SIKU TUKIWA KAMA WALIMU NA KAZI YETU HII NGUMU YA KUELIMISHA UMMA MZIMA WA WATANZANIA, ILI NASI TUSIMAME KWA MIGUU YETU NA KUACHANA NA KUITEGEMEA SERIKALI IMEPANDISHA MISHAHARA AU LA!
   ZIFUATAZO NI KANUNI 15 ZA KUZINGATIA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU KAMA WALIMU WA NCHI HII:-

  1. Usiwe mtumwa wa umaskini
  2. Usitake kujilinganisha na wengine
  3. Usifikirie sana mambo yaliyopita au kuhangaikia mambo yajayo
  4. Acha kulalamika
  5. Usiwe na moyo wa kuendeleza kinyongo
  6. Usiwe mtu wa kusubiri kufanya jambo fulani baadaye
  7. Acha kusema uongo
  8. Acha tabia ya kukwepa kufanya makosa
  9. acha kusema "SIWEZI"
  10. Acha kujifanya unajua kila kitu na huna shida na watu wengine
  11. Acha kufikiri kwamba hauko tayari kufanya jambo fulani
  12. Acha kujiwekea malengo madogo
  13. Usitake kila kitu ukifanye wewe
  14. Acha kununua vitu ambavyo huvihitaji
  15. Acha kuwalaumu watu wengine kwa matatizo yako
N/B:-
    Kumbuka:KAULI HII AMBAYO" MWALIMU MZOEFU DARASANI" HUPENDA      KUITUMIA "MUNGU PEKEE NDIYE NINAYEMWOGOPA,BINADAMU MWENZANGU NITAMHESHIMU TU"!!
    Mungu hakutuumba tuwe maskini bali sisi wenyewe ndiyo tunaoukaribisha umaskini kwa kusema SIWEZI wakati bosi wako akikuagiza kitu fulani ukifanye wakati hata yeye angeambiwa akifanye ASINGEWEZA......wala hukatai unaitikia tu kama mtumwa...usiwe mtumwa wa mawazo.Kama jambo huwezi kulitekeleza...sema bila mashaka kuwa "SIWEZI"
...........Leo huu ndo ushauri wangu.....!! Na "Mwalimu Mzoefu Darasani"


>> Maisha na kazi ni vitu viwili tofauti ni vema kama mwalimu fikiri kwa kina na fanya maamuzi sahihi kwa kujiamini na bila woga!
>>Walio wengi wanaamini kuwa kazi ya ualimu ni ya "Ndiyo bwana" sivyo kabisa hayo tunayataka wemyewe tuliyo ndani ya fani hii!!  
<<





BASI USIKOSE KUFUATANA NAMI KATIKA KUSAIDIA NA KUELIMISHANA JUU YA NAMNA YA KUYA-SHAPE MAISHA YETU YA KILA SIKU NA KUIPA HESHIMA FANI YETU........TCHAO!!