Thursday, July 3, 2014

"HEBU ...KAMA WALIMU TUZINGATIE HAYA MAMBO 15 KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU"

"WALIMU NA MAISHA YETU YA KILA SIKU:"
    SISI WALIMU KUTOKANA NA KAZI ZETU TUNAZOZIFANYA AMBAPO TUNAKOSA HATA MUDA WA KUFUATILIA MSTAKABARI WA MAISHA YETU NA FAMILIA ZETU,TUMEKUWA WEPESI SANA WA KUKATA TAMAA YA MAISHA AU KURAHISISHA MAISHA NA KUSALIA MIAKA NENDA MIAKA RUDI - TUKIRIDHIKA NA HALI YA MAISHA YA CHINI.
    MIMI KAMA "MWALIMU MZOEFU DARASANI" NATAKA NIKUPATIE KANUNI ZA MAISHA YETU YA KILA SIKU TUKIWA KAMA WALIMU NA KAZI YETU HII NGUMU YA KUELIMISHA UMMA MZIMA WA WATANZANIA, ILI NASI TUSIMAME KWA MIGUU YETU NA KUACHANA NA KUITEGEMEA SERIKALI IMEPANDISHA MISHAHARA AU LA!
   ZIFUATAZO NI KANUNI 15 ZA KUZINGATIA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU KAMA WALIMU WA NCHI HII:-

  1. Usiwe mtumwa wa umaskini
  2. Usitake kujilinganisha na wengine
  3. Usifikirie sana mambo yaliyopita au kuhangaikia mambo yajayo
  4. Acha kulalamika
  5. Usiwe na moyo wa kuendeleza kinyongo
  6. Usiwe mtu wa kusubiri kufanya jambo fulani baadaye
  7. Acha kusema uongo
  8. Acha tabia ya kukwepa kufanya makosa
  9. acha kusema "SIWEZI"
  10. Acha kujifanya unajua kila kitu na huna shida na watu wengine
  11. Acha kufikiri kwamba hauko tayari kufanya jambo fulani
  12. Acha kujiwekea malengo madogo
  13. Usitake kila kitu ukifanye wewe
  14. Acha kununua vitu ambavyo huvihitaji
  15. Acha kuwalaumu watu wengine kwa matatizo yako
N/B:-
    Kumbuka:KAULI HII AMBAYO" MWALIMU MZOEFU DARASANI" HUPENDA      KUITUMIA "MUNGU PEKEE NDIYE NINAYEMWOGOPA,BINADAMU MWENZANGU NITAMHESHIMU TU"!!
    Mungu hakutuumba tuwe maskini bali sisi wenyewe ndiyo tunaoukaribisha umaskini kwa kusema SIWEZI wakati bosi wako akikuagiza kitu fulani ukifanye wakati hata yeye angeambiwa akifanye ASINGEWEZA......wala hukatai unaitikia tu kama mtumwa...usiwe mtumwa wa mawazo.Kama jambo huwezi kulitekeleza...sema bila mashaka kuwa "SIWEZI"
...........Leo huu ndo ushauri wangu.....!! Na "Mwalimu Mzoefu Darasani"


>> Maisha na kazi ni vitu viwili tofauti ni vema kama mwalimu fikiri kwa kina na fanya maamuzi sahihi kwa kujiamini na bila woga!
>>Walio wengi wanaamini kuwa kazi ya ualimu ni ya "Ndiyo bwana" sivyo kabisa hayo tunayataka wemyewe tuliyo ndani ya fani hii!!  
<<





BASI USIKOSE KUFUATANA NAMI KATIKA KUSAIDIA NA KUELIMISHANA JUU YA NAMNA YA KUYA-SHAPE MAISHA YETU YA KILA SIKU NA KUIPA HESHIMA FANI YETU........TCHAO!!

No comments:

Post a Comment