Sunday, September 21, 2014

JUMAPILI NJEMA TENA YA KUABUDU BAADA YA MADHAMBI YA WIKI NZIMA

JAMBO KUBWA HAPA SI KUHUDHURIA KANISANI TU BALI NI IMANI NA MATENDO YAKO TU
  BINADAMU  WOTE TUMAEUMBWA NA MUNGU MMOJA,LAKINI ALICHOKITOFAUTISHA MUNGU KWETU NI ROHO NA AKILI YA KUTENDA MEMA AU MABAYA. BASI USIJITAZAME WEWE KWAMBA NI MCHA MUNGU KWA KUHUDHURIA KANISANI AU MSIKITINI BALI "UNATENDA YA KUPENDEZA MUNGU AU LA!
  DAIMA KANISANI TUNAKWENDA KUKUMBUSHWA TU KUWA TUSISAHAU KUTENDA MEMA KWANI SISI BINADAMU TU WASAHAULIFU NA WALA HATUENDI KANISANI KUPEWA MATENDO MEMA KWANI KUTENDA MEAMA AU MABAYA NI UAMUZI WA MTU MWENYEWE  KADRI AKILI NA ROHO YAKE INAVYOMTUMA
...........>>>>BASI LEO TUTAFAKARI HAYA NA DAIMA TUWE WATU KUTENDA MEMA NA SI KWENDA KANISANI KILA JUMAPILI NA MSIKITINI KILA IJUMAA KWA LENGO LA KUJIONESHA KWA WATU KUMBE AKILI NA ROHO ZETU HUTUTUMA KUTENDA MABAYA
>>>>>>>>>>>MBARIKIWE NYOTE MNAOTAMBUA KUWA KUWA MCHA MUNGU NI "MATENDO NA SI MANENO,MICHANGO KANISANI AU MSIKITINI,KUTOA MSAADA KWA KUWA UNA UWEZO NA KADHALIKA.!
                                             <<<<<<>>>>
................................Na Mwalimu Mzoefu Darasani..........................
 Mwl.Mzoefu Darasani na Ubavu wake!!!                                                         Na Obama na Ubavu wake!
                                                                                                                   

Saturday, September 20, 2014

TUJIULIZE KWA NINI TUNAFANYA KAZI KUTWA KUCHWA!

                        MI IMANI YANGU :
   NI KWA SABABU KAMA BABA AU MAMA TUNAWAJIBIKA KWA FAMILIA ZETU,HIVYO PILIKA ZOTE HIZI ZA KUSAKA PESA,MALI,UWEZO,VYEO,NYUMBA,MASHAMBA,ELIMU,AFYA,MAZINGIRA BORA,BIASHARA NA MENGINE MENGI YANAYOFANANA NA HAYO NI KWA SABABU YA KUZIJENGEA MAISHA BORA FAMILIA ZETU.
  BASI TUFANYE KAZI ZETU KWA MOYO,UADILIFU NA KWA KUMCHA MUNGU ILI TUWEZE KUFANIKIWA,KWANI KILA JAMBO UNALOFAMYA UKIMSHIRIKISHA MUNGU UNAWEZA!!
>>>>>>>>Na Mwalimu Mzoefu Darasani>>>>>>>!!

Wednesday, September 17, 2014

JALI AFYA YAKO

 UMEFANYA MAZOEZI ANGALAU MEPESI YA VIUNGO?
         KAMA KAWAIDA YANGU KAMA "MWL.MZOEFU DARASANI"KUKUPATIA DONDOO ZA AFYA,ELIMU NA IMANI.LEO NITUMIE FURSA HII KUKUKUMBUSHA KUWA AFYA NDIYO MAMBO YOTE.
        UKIUGUA,BASI UTAMBUE KUWA HATA KAMA UTAMWONA DAKTARI NI LAZIMA ATAITAZAMA AFYA YAKO KWA MAMBO MATATU NAYO NI:-
1.CHAKULA UNACHOKULA
2.MAZOEZI KAMA UNAFANYA
3.DAWA ULIZOWAHI KUTUMIA
         HATIMAYE ATAPENDEKEZA UANZE NA KIPI, KUMBUKA TIBA YA KWANZA KWA AFYA YA MIILI YETU NI"CHAKULA" IKIFUATIWA NA MAZOEZI YA VIUNGO NA DAWA ZA HOSPITALI NA HATUA YA MWISHO. BASI TUNALOPASWA KULIFAHAAMU HAPA NI "LIFE STYLE" YETU KATIKA LISHE YA KILA SIKU NDIYO ITAKAYOTUTAMBULISHA MWENENDO MZIMA WA AFYA ZETU.
          KAMA MWALIMU MZOEFU DARASANI NASHAURI YAFUATAYO:-
  • Tujali kupata chakula kuliko kitu kingine chochote-tena milo mitatu.
  • Tuupangilie muda wetu kwa wiki kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu.
  • Tusiwe watu wa kukimbilia kutumia dawa hata kwa ugonjwa unaoweza kutoweka kwa kufanya tu mazoezi
  • Tusipendelee sana starehe zitutawale daima-tufanye kazi ni sehemu ya mazoezi.
  • Basi ukitaka mipango na maisha yako yote yaharibike, chezea afya kwa kutafuta magonjwa-"Bakia njia kuu"
<<<<<<<< Ni ushauri tu ....Na "Mwl Mzoefu Darasani">>>>>>>>

Monday, September 15, 2014

VIJANA WAKO NYUMBANI BAADA YA MITIHANI YAO YA TAR.10/9 HADI 11/9

          WATU WANASEMA "MUNGU NA MBIO"
   Tunashukuru mitihani imemalizika bila mizengwe,na sasa sisi kama wadau wa fani hii tunachokifanya ni kufanya maombezi yake kwa Mola ili watoto wetu waibuke na ushindi na kushinda mitihani hiyo na hatimaye kutimiza ndoto zao za kwenda sekondari-ndiyo malengo yetu sisi wadau na hasa "Mwalimu Mzoefu" Si unajua tena hii ndo fani aliyonipatia Mwenyezi Mungu lazima niitendee haki kwa wanadamu wanaonipatia watoto wao na kuniamini>>> Basi tuungane pamoja kuwaombea vijana wetu!!
!!!.................Na Mwalimu Mzoefu Darasani..............!!!  
 
 Walimu kazi yetu tumeifanya kwa moyo na uhodari mkubwa na sasa Baba wa wote ndiye mweny "maamuzi"....!!! 

Tuesday, September 9, 2014

MITIHANI - MITIHANI - MITIHANI -DRS VII HIYOOO!!

MIMI NISEME KAMA MWL MZOEFU DARASANI MAANDALIZI YALIKUWA MAZURI NA HASA KWA WANAFUNZI WA S/M MISUNKUMILO WILAYA YA MPANDA - MKOA WA KATAVI
            VIJANA WAPO TAYARI KWA MITIHANI HII NA NIMATUMAINI YANGU MAKUBWA WATOTO WATAFANYA VIZURI ,UKIZINGATIA NAMI NILIKUWA MIONGONI MWA TIMU ILIYOKUWA IKIWANOA WATOTO WA S/M MISUNGUMILO WALIOKUWEPO KAMBINI KWA TAKRIBANI SIKU 21
            WAKATI HUO HUO KAMBI YAO ILIFUNGWA RASMI NA AFISA ELIMU WA H/SHAURI YA MJI WA MPANDA BW, KAYOMBO KWA DUA, NASAHA, MAOMBI NA KUTOA MOTISHA KWA WANAFUNZI NA WALIMU WAO

Hapa chini wanafunzi wakiwa katika hekaheka za mwisho leo asubuhi shuleni Misunkumilo>>>>Tazama:>>