Tuesday, November 18, 2014

NJORUMLI~NJORUMLI~NJORUMLI [NJOMBE,RUVUMA,MTWALA NA LINDI] -

NJORUMLI - Ni kifupi sha mikoa ya [Njombe,Ruvuma,Mtwara,Lindi]
   Umoja huu ulianzishwa miaka mitatu iliyopita kwa madhumuni yafuatayo:-
  • Kufahamiana watu wa nyumbani tunaoishi mkoani Katavi
  • Kujenga udugu,upendo na ushirikiano katika mambo mbalimbali
  • Kufarijiana katika misiba
  • Kushirikiana katika mambo ya furaha k.v.harusi
  • Kutoa mikopo midogomidogo kwa ajili ya ujasiliamali
   Mwanachama wa umoja huu ni yule mwenye sifa zifuatazo:-
  1. Anayetoka mikoa iliyotajwa hapo juu
  2. Aliyeolewa au kuoa toka mikoa hiyo
  3. Aliyewahi kuwa mgeni rasmi katika sherehe zetu akipenda (k.m Mr Dhallah na Kpufi ni wa
    nachama)
Aidha tuna katiba yetu inayotuongoza, na iliyoweka masharti ya namna ya kujiunga,manufaa,michango n.k. Ukitaka kujiunga utafuata taratibu hizi tatu:-
  1. Toa kiingilio sh.5,000/-
  2. Nunua katiba sh.3,700/-
  3. Utalipa ada ya kila mwezi sh.2,000/-
N/B:- Hudhuria vikao vya kila mwezi,ili kudhihirisha uhai wako katika chama.
Basi maelezo na ufafanuzi huu mfupi,unakaribishwa sana kuungana nasi ili kujega mshiksmsno na kujiinua kiuchumi kwa kubadilishana mawazo na kuendesha biashara ndogondogo - bado hujachelewa.
MAWASILIANO:
Ukitaka kutupata tumia,
   Simu: 0784431651 - Katibu
   Email:anaclethaule@yahoo.co.uk
   Blog ya "Mwalimu Mzoefu Darasani" - Utapata kuziona picha mbalimbali za wanachama
UNAKARIBISHWA KUJIUNGA>>>>!!
<<<<<<<<<<>>>>>>>>>!!

Tuesday, November 4, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA JUU YA NJORUMLI - MPANDA, KATAVI:

KIONGOZI WA NJORUMLI( WATU WATOKAO NJOMBE,RUVUMA,MTWARA NA LINDI) AKIWA PAMOJA NA MFADHIRI WA UMOJA HUO KATIKA MAKABIDHIANO YA ZAWADI YA FEDHA ALIYOIAHIDI MFADHIRI HUYO NDG.SEBASTIAN KAPUFI KATIKA HAFLA YA KUUKARIBISHA MWAKA HUU HAPO JANUARI MWAKA HUU.
Wa kushoto ni Ndg Kapufi akikabidhi fedha.

Ukulia ni M/kiti Ngonyani akihesabu fedha
Katibu -Mwl. Haule
Makabidhiano ya zawadi toka kwa Sebastian Kapufi -Nyumbani kwake Nsemulwa (Picha na Mwl.Mzoefu Darasani)

MARAFIKI WA RADIO MARIA (MRMT)-MPANDA CLUB

KARIBUNI KATIKA CLUB YETU YA MARAFIKI WA RADIO MARIA ILIYOPO KIGANGO CHA MWANGAZA JIMBO LA MPANDA-ILYOANZISHWA RASMI TAREHE 10-03-2014 CHINI YA USIMAMIZI WA ELIAS MILWANO NA STANSLAUS MHEMA WA RM MAKAO MAKUU, IKIWA NA WANACHAMA 17.
   LEO TAREHE 01-11-2014 KATIKA IBADA YAO YA KILA MWANZO WA MWEZI NGAZI YA KIGANGO IMETOA VITAMBULISHO RASMI KWA BAADHI YA WANACHAMA WAO NA KUCHANGIA RM SH.18,000/- HAWA NI BAADHI YA WANA- KLABU WALIOPATIWA VITAMBULISHO HIVYO WAKIONGOZWA NA MUHAMASISHAJI WAO PICHA YA CHINI.
<<<<>>>>>>!!
Club ya MRMT-Mpanda
Mhamasishaji Mwl Haule
Waumini wa kanisa la Ilembo-Mpanda
Kanisa la Hija Parokia ya Ilembo-Mpanda

Wana-kwaya Parokia ya Ilembo