Tuesday, November 18, 2014

NJORUMLI~NJORUMLI~NJORUMLI [NJOMBE,RUVUMA,MTWALA NA LINDI] -

NJORUMLI - Ni kifupi sha mikoa ya [Njombe,Ruvuma,Mtwara,Lindi]
   Umoja huu ulianzishwa miaka mitatu iliyopita kwa madhumuni yafuatayo:-
  • Kufahamiana watu wa nyumbani tunaoishi mkoani Katavi
  • Kujenga udugu,upendo na ushirikiano katika mambo mbalimbali
  • Kufarijiana katika misiba
  • Kushirikiana katika mambo ya furaha k.v.harusi
  • Kutoa mikopo midogomidogo kwa ajili ya ujasiliamali
   Mwanachama wa umoja huu ni yule mwenye sifa zifuatazo:-
  1. Anayetoka mikoa iliyotajwa hapo juu
  2. Aliyeolewa au kuoa toka mikoa hiyo
  3. Aliyewahi kuwa mgeni rasmi katika sherehe zetu akipenda (k.m Mr Dhallah na Kpufi ni wa
    nachama)
Aidha tuna katiba yetu inayotuongoza, na iliyoweka masharti ya namna ya kujiunga,manufaa,michango n.k. Ukitaka kujiunga utafuata taratibu hizi tatu:-
  1. Toa kiingilio sh.5,000/-
  2. Nunua katiba sh.3,700/-
  3. Utalipa ada ya kila mwezi sh.2,000/-
N/B:- Hudhuria vikao vya kila mwezi,ili kudhihirisha uhai wako katika chama.
Basi maelezo na ufafanuzi huu mfupi,unakaribishwa sana kuungana nasi ili kujega mshiksmsno na kujiinua kiuchumi kwa kubadilishana mawazo na kuendesha biashara ndogondogo - bado hujachelewa.
MAWASILIANO:
Ukitaka kutupata tumia,
   Simu: 0784431651 - Katibu
   Email:anaclethaule@yahoo.co.uk
   Blog ya "Mwalimu Mzoefu Darasani" - Utapata kuziona picha mbalimbali za wanachama
UNAKARIBISHWA KUJIUNGA>>>>!!
<<<<<<<<<<>>>>>>>>>!!

No comments:

Post a Comment