Tuesday, November 24, 2015

MWALIMU MZOEFU DARASANI-LEO NA MITIHANI YA DARASA LA IV -KITAIFA;

UNAJUA NINI...AMBACHO HUKIJUI JUU YA MITIHANI YA DARASA LA IV!!
  • Wadau wanauandaa mtihani huu kwa mazoea tu kwa sababu bajeti yake ni ya kubabaisha na wakati mwingine shule zinalazimika kuchangia uendeshaji wake.
  • Wadau hawawaandai watahiniwa kama wale wa darasa la vii
  • Walimu wakuu unafika wakati wa kupambana na wazazi/walezi juu ya michango ya chakula kwa wanafunzi kwa siku mbili za mtihani-hii ni pamoja na kuwalipa wapishi
  • Watahiniwa hawaandaliwi kisaikolojia ikiwa ni pamoja kuwapatia viwango vya kitaifa vya ufaulu wa mitihani hii-hivyo mtahiniwa husalia gizani asielewe kuwa asipofanya nini kitatokea
  • Kutokana na uhafifu wa umuhimu wa mtihani huu-imefikia hata mzazi/mlezi hajawahi kushuhudia mtoto wake akikariri darasa kwa kushindwa mtihani huu na ndio maana hawajibiki ipasavyo kwa mtoto wake na wala shughuli zote zihusuzo mitihani hii kwa ujumla
  • Matokeo ya hayo yote-ni KUUONA MTIHANI HUU NI KAMA MILA NA DESTURI IKIFIKA MUDA WAKE BASI TUANDAE WATOTO WAKAFANYE....BASI!!
<><><><>Ni mtazamo wangu kama Mwl Mzoefu Darasani<><><><>!!!!!
NITUMIE NAFASI HII KUWATAKIA KILA LA KHERI WAANDAJI-WASIMAMIZI-NA WATAHINIWA WOTE-MTIHANI MWEEEEEMAAAAA!!!
<><><>Na MMD-S/M-M/MILO<><><>!!


 








Mwl Mzoefu Darasani(MMD)

Tuesday, November 17, 2015

LEO NA MWL MZOEFU DARASANI(MMD)....!!

NGOJA........NIZUNGUMZIE HII MITIHANI YA DARASA LA NNE KITAIFA TUNAYOIENDESHA NA KUISIMAMIA KILA MWAKA.
.......>>NIZUNGUMZIE UBORA WAKE NA UMUHIMU WAKE:
1.Umepungua kwa kiasi kikubwa:
  • Fedha za kuendeshea zinapunguzwa siku baada ya siku ..na huko tunakokwenda utatokea kuanza kuwachangisha wazazi
2.Hauna kiwango maalum cha ufaulu ..matokeo yake kila mwalimu mkuu anakiwango chake cha kuwapeleka watoto hao darasa la tano:
  • Kwa ujumla watoto hao wafaulu wasifaulu wanaingia darasa kama kawaida wala hakuna mdau yeyote anayeshituka na kukumbuka kuwa malengo ya mtihani huu ni kuwapima watoto na kuwachuja ili darasa la tano waingie kwa kichwa na si kwa miguu(waingie wenye uwezo tu)
  • Hakuna inayofuatilia wanafunzi walioingia darasa la tano baada ya mtihani...si wadau wa mkoa,wilaya wala kata- kazi inasalia kwa m/mkuu peke yake
3.Swali hapa na hoja kuu ni nani awajibike:
  • Wizara-haiupatii mtihani huu umuhimu unaostahili?
  • Maafisa elimu mikoa -  hawaoni umuhimu wake lakini wanaona fedha toka wizarani hivyo wazifanyie kazi zisirudishwe?
  • Maafisa elimu wilaya - wanapokea maagizo tu basi?
  • Waratibu elimu kata - wamezoea kuona mitihani hii ikifanyika kila mwaka na hivyo hawana haja ya kuuliza kama wanachokisimamia ni sahihi au la!?
  • Walimu wangu wakuu - wenye kupokea kama yalivyo hata kama hayajaiva...wanauzoefu wa kuyarudisha katika jiko mpaka yaive na kuliwa na wanafunzi wao?
MPAKA HAPO SINA MAELEZO MAZURI ZAIDI KAMA MWL MZOEFU DARASANI! ..NINACHOSHAURI KWA UZOEFU WANGU NI KWAMBA TUSIMAMIE MITIHANI YA SHULE VIZURI TU INATOSHA MBONA ENZI ZETU TULIKUWA TUKIFANYA VIZURI PASIPO MITIHANI HII?>>>>>>>>SIJUI WEWE UNA MAONI GANI YENYE MSAADA ZAIDI ....Toa maoni yako>>>...!!
              <<<<<
Darasa>>


 Boss wa elimu
<<                           















                                      MMD - Kulia>