.......>>NIZUNGUMZIE UBORA WAKE NA UMUHIMU WAKE:
1.Umepungua kwa kiasi kikubwa:
- Fedha za kuendeshea zinapunguzwa siku baada ya siku ..na huko tunakokwenda utatokea kuanza kuwachangisha wazazi
2.Hauna kiwango maalum cha ufaulu ..matokeo yake kila mwalimu mkuu anakiwango chake cha kuwapeleka watoto hao darasa la tano:
- Kwa ujumla watoto hao wafaulu wasifaulu wanaingia darasa kama kawaida wala hakuna mdau yeyote anayeshituka na kukumbuka kuwa malengo ya mtihani huu ni kuwapima watoto na kuwachuja ili darasa la tano waingie kwa kichwa na si kwa miguu(waingie wenye uwezo tu)
- Hakuna inayofuatilia wanafunzi walioingia darasa la tano baada ya mtihani...si wadau wa mkoa,wilaya wala kata- kazi inasalia kwa m/mkuu peke yake
3.Swali hapa na hoja kuu ni nani awajibike:
- Wizara-haiupatii mtihani huu umuhimu unaostahili?
- Maafisa elimu mikoa - hawaoni umuhimu wake lakini wanaona fedha toka wizarani hivyo wazifanyie kazi zisirudishwe?
- Maafisa elimu wilaya - wanapokea maagizo tu basi?
- Waratibu elimu kata - wamezoea kuona mitihani hii ikifanyika kila mwaka na hivyo hawana haja ya kuuliza kama wanachokisimamia ni sahihi au la!?
- Walimu wangu wakuu - wenye kupokea kama yalivyo hata kama hayajaiva...wanauzoefu wa kuyarudisha katika jiko mpaka yaive na kuliwa na wanafunzi wao?
MPAKA HAPO SINA MAELEZO MAZURI ZAIDI KAMA MWL MZOEFU DARASANI! ..NINACHOSHAURI KWA UZOEFU WANGU NI KWAMBA TUSIMAMIE MITIHANI YA SHULE VIZURI TU INATOSHA MBONA ENZI ZETU TULIKUWA TUKIFANYA VIZURI PASIPO MITIHANI HII?>>>>>>>>SIJUI WEWE UNA MAONI GANI YENYE MSAADA ZAIDI ....Toa maoni yako>>>...!!
Boss wa elimu
<<
MMD - Kulia>
No comments:
Post a Comment