Tuesday, November 24, 2015

MWALIMU MZOEFU DARASANI-LEO NA MITIHANI YA DARASA LA IV -KITAIFA;

UNAJUA NINI...AMBACHO HUKIJUI JUU YA MITIHANI YA DARASA LA IV!!
  • Wadau wanauandaa mtihani huu kwa mazoea tu kwa sababu bajeti yake ni ya kubabaisha na wakati mwingine shule zinalazimika kuchangia uendeshaji wake.
  • Wadau hawawaandai watahiniwa kama wale wa darasa la vii
  • Walimu wakuu unafika wakati wa kupambana na wazazi/walezi juu ya michango ya chakula kwa wanafunzi kwa siku mbili za mtihani-hii ni pamoja na kuwalipa wapishi
  • Watahiniwa hawaandaliwi kisaikolojia ikiwa ni pamoja kuwapatia viwango vya kitaifa vya ufaulu wa mitihani hii-hivyo mtahiniwa husalia gizani asielewe kuwa asipofanya nini kitatokea
  • Kutokana na uhafifu wa umuhimu wa mtihani huu-imefikia hata mzazi/mlezi hajawahi kushuhudia mtoto wake akikariri darasa kwa kushindwa mtihani huu na ndio maana hawajibiki ipasavyo kwa mtoto wake na wala shughuli zote zihusuzo mitihani hii kwa ujumla
  • Matokeo ya hayo yote-ni KUUONA MTIHANI HUU NI KAMA MILA NA DESTURI IKIFIKA MUDA WAKE BASI TUANDAE WATOTO WAKAFANYE....BASI!!
<><><><>Ni mtazamo wangu kama Mwl Mzoefu Darasani<><><><>!!!!!
NITUMIE NAFASI HII KUWATAKIA KILA LA KHERI WAANDAJI-WASIMAMIZI-NA WATAHINIWA WOTE-MTIHANI MWEEEEEMAAAAA!!!
<><><>Na MMD-S/M-M/MILO<><><>!!


 








Mwl Mzoefu Darasani(MMD)

No comments:

Post a Comment