Busara huhitajika hata kama una elimu yako

SIKU HIZI ZA KARIBUNI UMEWAHI KUSHUHUDIA NA UNAENDELEA KUSHUHUDIA:
- WATU WANAVAA VIZURI
- WATU WANAVAA NUSU UCHI
- WATU WANAPIGA PICHA ZENYE UBORA WA HALI YA JUU
- WATU WANAPIGA PICHA ZA UTUPU
- WATU WANAONGEA KIINGEREZA KIZURI
- WATU WANAONGEA KISWA-NGLISH
- WATU WANAINGIA KATIKA SIASA KWA WINGI
- WATU WANACHANGIA VURUGU/MTAFARUKU BUNGENI
- WATU WANAANZISHA SHULE ZA UHAKIKA
- WATU WANAANZISHA SHULE KAMA UYOGA MAHALI POPOTE
- NA MENGINE MENGI YANAYOFANANA NA HAYO!!
UNAJUA SABABU YA HAYA YOTE?
Watu wamefika mahali na kuonekana hakuna asiyesoma hapa Tanzania.....na kwa maana hiyo kuonekana aliyesoma ni kama hajasoma na asiyesoma ni kama ana elimu zaidi ya elimu....na kwa kukuhakikishia kuwa yeye ameelimika basi anafungua na mitandao na kuiga kila kitu anachokiona humo-Matokeo yake,na yule aliyesoma kiuhakika ili asipitwe na huyo mpumbavu-mwenye elimu zaidi ya elimu basi naye anajiingiza katika mkumbo huo wa kuiga kila kitu ili amshshinde yule mwenye elimu zaidi ya elimu.
Ndiyo maana leo hii mitandaoni utashuhudia:
- WASOMI NA WASIO WASOMI
- MAARUFU NA WASIO MAARUFU
- WANASIASA NA WASIO WANASIASA
- VIONGOZI NA WASIO VIONGOZI
- WALIMU NA WASIO WALIMU
- WANAFUNZI NA WASIO WANAFUNZI
- WALEMBO NA WASIO WALEMBO
- WASANII NA WASIO WASANII
- WATANGAZAJI NA WASIO WATANGAZAJI
- NA WENGINE KAMA HAO
Wakifanya vituko vinavyowashangaza watanzania kila kukicha --utashuhudia katika:
- RUNINGA
- REDIO
- MAGAZETI
- MITANDAO
- SIMU-UJUMBE MFUPI
N/B:-MWALIMU - MZOEFU DARASANI - NASEMA HIVI:
"WATU SIKU HIZI WANASOMA SANA LAKINI HAWAELIMIKI"- HILI NDILO TATIZO
TULILONALO KWA SASA!
Huu ni mtazamo wangu tu>>>> Kama Mwalimu Mzoefu Darasani>>>!!

Uzoefu unaonesha,elimu huanzia nyumbani kwa baba na mama-mwalimu anafuatia tu!