Achana na katiba na mambo yake,achana na ukawa na mambo yake,achana na ahadi za kupanda kwa kima cha chini cha mishahara mimi nazungumzia namna gani mwanafunzi anavyoweza kufaulu mtihani wake wa mwisho:
1.Ajiandae vizuri katika mitihani yake ya majaribio k.v.mitihani ngazi ya shule,kata,wilaya na mkoa.
2.Kila siku ahudhuriapo shuleni ajiwekee ratiba yake binafsi k.m,leo nitasoma somo fulani
3.Ashirikiane na wenzake kupata kile ambacho yeye hana.
4.Aombe msaada kwa mwalimu wake pale tu darasa zima linapokosa jibu kwa swali lake.
Ni ushauri tu..........kwa wanafunzi na walimu wenzangu wanaofundisha darasani>>>>>!!
Na mwalimu mzoefu darasani .....!!!
No comments:
Post a Comment