Thursday, December 25, 2014

X-MAS NA MWALIMU MZOEFU DARASANI>>>>

MPANDA-KATAVI MAMBO YAMEKWENDA SALAMA LAKINI......!!
MH. MTOTO WA MKULIMA AMESHEREHEKEA NYUMBANI KWAKE KIJIJINI,MIMI MWL MZOEFU DARASANI(MMD),NIMEKESHA MSIBANI-ENEO LA MADUKANI -HAPA MJINI MPANDA,WENGINE KANISANI,WENGINE,HOSPITALINI,WENGINE BIASHARA NDO ZILICHANGANYA,KUKU NDO ZLIKUWA WAHANGA WA SHEREHE,MAOVU YA HAPA NA PALE HAYAKUKOSEKANA, ILI MRADI KILA BINADAMU NA MAPENDELEO YAKE.
             LAKINI HAYO YOTE NI MALIMWENGU TU, KITU CHA MSINGI WEWE NA MIMI KAMA NI WAUMINI  TUJIULIZE TULIJIANDAAJE KIROHO KUMPOKEA MKOMBOZI WETU YESU KRISTO?>>>TUTAFAKARI JAMBO HILI WAUMINI WOTE WA KIKRISTO>>>>
+++++Na: Mwl Mzoefu Darasani(mmd)++++
KanisaniWana-kwaya

Tuesday, December 9, 2014

USINGOJE MTU AKUPONGEZE KWA MAFANIKIO YAKO MWENYEWE ~ JIPONGEZE MWENYEWE:NDICHO WALICHOKIFANYA S/M MISUNKUMILO TAREHE 08.12.2014:

WALIMU WA S/M MISUNKUMILO WAJIPONGEZA KWA MATOKEO MAZURI YA DRS VII KWA ASILIMIA 92.
~~~~JANA ILIKUWA NI SIKU YA MIKIKI-MIKIKI MINGI KWA WALIMU WAS/M M/MILO KUTOKANA MAANDALIZI YA MWISHO MWISHO KUINGIA UKUMBI WA WHITE CLUB TAYARI KWA KUJIPONGEZA KWA KAZI YA MWAKA MZIMA ILIYO NZURI NA YENYE MAFANIKIO MAKUBWA.
~~~~WANAFUNZI WALIOFANYA MTIHANI WA DARASA LA SABA TAIFA WALIKUWA 51 KWA MUJIBUWA MWALIMU MKUU, NA VIJANA 47 WAMECHAGULIWA KUENDELEA NA SEKONDARI, NA KUFANYA ASILOMIA 92 YA WATAHINIWA WOTE AIDHA WALIOSHINDWA MTIHANI HUO NI VIJANA WANNE(4) TU. HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA!!
~~~~PAMOJA NA KUJIPONGEZA VILEVILE NILISHUHUDIA KUWAANGA WALIMU WALIMU WALIOTEULIWA KUSHIKA NYADHIFA MBALIMBALI NA KUWAKARIBISHA WALE WALIOHAMIA  KWA LENGO LA KZIBA PENGO WALE WALIOONDOKA.AIDHA ILIPIGWA KARAMBEE MOJA KALI YA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA UPATIKANAJI WA KOMPYUTA NA PRINTER.
~~~~HARAMBEE ILIYOONGOZWA NA Ndg KAYOMBO AFISA ELIMU MJI AKISAIDIA NA AFISA ELIMU TAALUMA MJI Ndg PILI-KWA KWELI MAMBO YALINOGA, KWANI TSH.800,000 ZILIKUSANYWA IKIWA NI TASLIMU NA AHADI KATI YA LENGO LA TSH.1,000,000/- ZINAZOHITAJIKA.~~HAPA CHINI PATA HABARI KAMILI KWA NJIA YA PICHA NA VIDEO.
                                             >>>>>>Na Mwalimu Mzoefu Darasani>>>>

Wednesday, December 3, 2014

MWISHO WA MWAKA UNA MAMBO YAKE - HEBU FUNGUA UONE MPANDA WANAVYOJIANDAA NA TAALUMA YA H/MJI MWAKA 2015

ELIMU BORA YATAKA MAANDALIZI BORA - H/MJI MPANDA HAPA YAFANYA YAO!!
>>>Bwana Afisa Elimu Mr. Kayombo amefanya mabadiliko ya uongozi wa shule za msingi katika H/Mji Mpanda kwa kuwateua walimu wakuu wapya,wasaidizi na walimu wengine kuwahamisha kutoka kituo kimoja cha kazi hadi kingine kwa lengo la kuziba mapengo au kuimarisha au kusawazisha ikama za shule zake wilayani hapa.
>>>Baadhi ya waliokumbwa na uhamisho huo ni pamoja na :
  • Mwl.Tweve - toka s/m Misunkumilo
  • Mwl.Maico - toka s/m Misunkumilo
  • Mwl Mdeda - toka s/m Misunkumilo
  • Mwl.Kisaye - toka s/m Mwangaza
  • Mwl.Innocent - toka s/m Makanyagio
  • Mwl.Denis - toka s/m Kashato
  • Mwl.Sophia - toka s/m Katavi
  • Mwl.Masai - toka s/m Nsemulwa
  • Mwl.Peleka - toka s/m Mapinduzi
  • Mwl. Medda - toka s/m Kashato
  • Mwl. Kissa - toka s/m Nsemulwa n.k.
Ni baadhi tu ya waliohama kwa kushika madaraka k.v. Uratibu,M/Mkuu na M/M/Msaidizi,lengo la Afisa elimu huyu ni kuisuka timu yake kabambe tayari kwa mapambano ya mwakani 2015 kwa darasa la saba,ukizingatia kuilinda nafasi tuliyoipata mwaka huu kunyakua nafasi ya kwanza kwa H/Miji yote Tanzania.
<<<<
!!!!!!!!!!!!!!!!!!Na Mwl.Mzoefu Darasani!!!!!!!!!!!!!!!!!!! 
Mwl Mzoefu Darasani!!

Tuesday, November 18, 2014

NJORUMLI~NJORUMLI~NJORUMLI [NJOMBE,RUVUMA,MTWALA NA LINDI] -

NJORUMLI - Ni kifupi sha mikoa ya [Njombe,Ruvuma,Mtwara,Lindi]
   Umoja huu ulianzishwa miaka mitatu iliyopita kwa madhumuni yafuatayo:-
  • Kufahamiana watu wa nyumbani tunaoishi mkoani Katavi
  • Kujenga udugu,upendo na ushirikiano katika mambo mbalimbali
  • Kufarijiana katika misiba
  • Kushirikiana katika mambo ya furaha k.v.harusi
  • Kutoa mikopo midogomidogo kwa ajili ya ujasiliamali
   Mwanachama wa umoja huu ni yule mwenye sifa zifuatazo:-
  1. Anayetoka mikoa iliyotajwa hapo juu
  2. Aliyeolewa au kuoa toka mikoa hiyo
  3. Aliyewahi kuwa mgeni rasmi katika sherehe zetu akipenda (k.m Mr Dhallah na Kpufi ni wa
    nachama)
Aidha tuna katiba yetu inayotuongoza, na iliyoweka masharti ya namna ya kujiunga,manufaa,michango n.k. Ukitaka kujiunga utafuata taratibu hizi tatu:-
  1. Toa kiingilio sh.5,000/-
  2. Nunua katiba sh.3,700/-
  3. Utalipa ada ya kila mwezi sh.2,000/-
N/B:- Hudhuria vikao vya kila mwezi,ili kudhihirisha uhai wako katika chama.
Basi maelezo na ufafanuzi huu mfupi,unakaribishwa sana kuungana nasi ili kujega mshiksmsno na kujiinua kiuchumi kwa kubadilishana mawazo na kuendesha biashara ndogondogo - bado hujachelewa.
MAWASILIANO:
Ukitaka kutupata tumia,
   Simu: 0784431651 - Katibu
   Email:anaclethaule@yahoo.co.uk
   Blog ya "Mwalimu Mzoefu Darasani" - Utapata kuziona picha mbalimbali za wanachama
UNAKARIBISHWA KUJIUNGA>>>>!!
<<<<<<<<<<>>>>>>>>>!!

Tuesday, November 4, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA JUU YA NJORUMLI - MPANDA, KATAVI:

KIONGOZI WA NJORUMLI( WATU WATOKAO NJOMBE,RUVUMA,MTWARA NA LINDI) AKIWA PAMOJA NA MFADHIRI WA UMOJA HUO KATIKA MAKABIDHIANO YA ZAWADI YA FEDHA ALIYOIAHIDI MFADHIRI HUYO NDG.SEBASTIAN KAPUFI KATIKA HAFLA YA KUUKARIBISHA MWAKA HUU HAPO JANUARI MWAKA HUU.
Wa kushoto ni Ndg Kapufi akikabidhi fedha.

Ukulia ni M/kiti Ngonyani akihesabu fedha
Katibu -Mwl. Haule
Makabidhiano ya zawadi toka kwa Sebastian Kapufi -Nyumbani kwake Nsemulwa (Picha na Mwl.Mzoefu Darasani)

MARAFIKI WA RADIO MARIA (MRMT)-MPANDA CLUB

KARIBUNI KATIKA CLUB YETU YA MARAFIKI WA RADIO MARIA ILIYOPO KIGANGO CHA MWANGAZA JIMBO LA MPANDA-ILYOANZISHWA RASMI TAREHE 10-03-2014 CHINI YA USIMAMIZI WA ELIAS MILWANO NA STANSLAUS MHEMA WA RM MAKAO MAKUU, IKIWA NA WANACHAMA 17.
   LEO TAREHE 01-11-2014 KATIKA IBADA YAO YA KILA MWANZO WA MWEZI NGAZI YA KIGANGO IMETOA VITAMBULISHO RASMI KWA BAADHI YA WANACHAMA WAO NA KUCHANGIA RM SH.18,000/- HAWA NI BAADHI YA WANA- KLABU WALIOPATIWA VITAMBULISHO HIVYO WAKIONGOZWA NA MUHAMASISHAJI WAO PICHA YA CHINI.
<<<<>>>>>>!!
Club ya MRMT-Mpanda
Mhamasishaji Mwl Haule
Waumini wa kanisa la Ilembo-Mpanda
Kanisa la Hija Parokia ya Ilembo-Mpanda

Wana-kwaya Parokia ya Ilembo

Tuesday, October 7, 2014

MWALIMU NA UALIMU!!

KUWA MWALIMU SI KAZI BALI UALIMU NI KAZI NGUMU SANA:-
   Unajua ukichukua jukumu tu la kuwafundisha wenzako tayari utaitwa "Mwalimu" lakini huna cheti rasmi cha kazi hiyo, hivyo ndivyo unavyoweza kuitwa Mwalimu.
   Sasa ualimu sio hivyo unavyodhani.Ualimu ni matendo yote mwalimu anayopaswa kuandaa kabla hajaingia darasani na hayo ndiyo mwalimu huyu anapaswa kuyasomea na kisha kuyafanyia kazi ili kuitendea haki fani hii.
   Hakika ugumu wa kazi hii umekalia pale ambapo kila unapotaka kumpatia mwanafunzi ufahamu wa namna yoyote ile ni lazima ufuate taratibu zote. taratibu hizo ni pamoja na:-
  1. Kuandaa somo
  2. Kuandaa maelezo mafupi (Notes)
  3. Kuandaa zana za kufundishia
  4. Kuingia darasani na kuanza kufuatilia ufundishaji kama ulivyoandaa - yaani kwa kufuata kipengele kwa kipengele muda kwa muda na mwisho kumpatia kazi ya kufanya mwanafunzi na kusahihisha kazi yake
  5. Kazi za kufanya baada ya kutoka darasani ni pamoja na;-
  • Kumalizia kusahihisha
  • Kuandika tathmini na maoni
  • Kujaza daftari la uthibitisho kama umefundisha(Class log book)
  • Kujaza daftari la mada uliyofundisha/shajara (Subjects log book) 
Taratibu hizi na zile ambazo sijazitaja zifanywe kwa kila somo unalokwenda kulifundisha siku hiyo-sasa hiyo ni tisa kumi kwa siku mwalimu ana masomo zaidi ya matano kulingana na uchache wa walimu katika shule husika anayopaswa kuyafundisha na kufuata taratibu zote nilizozieleza hapo juu
   Sema sasa, Je, mwalimu unaweza kumwekea kipimo cha ufundishaji wake kwa siku? Hapana, kinachofanyika ni kuwa,mwingine ataonesha bidii na mwingine atategea.! Lakini mwisho wa mwezi mshahara wa mtegaji na mchapa kazi hakuna tofauti!!
USHAURI:
  Kama -"Mwalimu Mzoefu Darasani" nashauri ,ili Mchapakazi asikatishwa tamaa na Mtegaji - Serikali iandae malipo ya ziada (Bonasi) kwa mwalimu anayetimiza majukumu yake barabara mara tu baada ya wakaguzi wa shule kuthibitisha hilo - Kwa utafiti wangu nimegundua wakaguzi wakikagua utasikia wakisema - mwalimu huyu ana asilimia 80 na mwingine asilimia 30 na wanaishia kusifu tu kwa maneno aliyefanya vizuri na kumkemea yule aliyefanya vibaya zoezi huishia hapo. - Hapo mimi sijaona motisha iko wapi....Kwa leo inatosha - siku nyingine Tchao!!
              >>>>>>>Na "Mwalimu Mzoefu Darasani">>>>>>> 
             

MWALIMU NA UALIMU

MWALIMU NA UALIMU

Monday, October 6, 2014

JUMATATU - SIKU YA KAZI

TUKICHAPA KAZI KWA NIA NA MALENGO TUTAONGEZA KIPATO CHETU NA TAIFA KWA UJUMLA.TUCHAPE KAZI KWA MOYO NA UPENDO WA KUWAHUDUMIA WENZETU.


IPENDE KAZI YAKO KWANI HUKULAZIMISHWA KUIFANYA.KUMBUKA KUWA MZALENDO KWA NCHI YAKO KAMA WENZETU ULAYA NA MAREKANI WANAVYOITETEA NCHI YAO KWA HALI NA MALI - TUWE HIVYO SI KILA KUKICHA NI LAWAMA TU ! HEBU TUFANYE KAZI TUONE KAMA HATUTALETA MABADILIKO!!









........Ni ushauri tu ....na Mwalimu Mzoefu Darasani........!!!

Sunday, September 21, 2014

JUMAPILI NJEMA TENA YA KUABUDU BAADA YA MADHAMBI YA WIKI NZIMA

JAMBO KUBWA HAPA SI KUHUDHURIA KANISANI TU BALI NI IMANI NA MATENDO YAKO TU
  BINADAMU  WOTE TUMAEUMBWA NA MUNGU MMOJA,LAKINI ALICHOKITOFAUTISHA MUNGU KWETU NI ROHO NA AKILI YA KUTENDA MEMA AU MABAYA. BASI USIJITAZAME WEWE KWAMBA NI MCHA MUNGU KWA KUHUDHURIA KANISANI AU MSIKITINI BALI "UNATENDA YA KUPENDEZA MUNGU AU LA!
  DAIMA KANISANI TUNAKWENDA KUKUMBUSHWA TU KUWA TUSISAHAU KUTENDA MEMA KWANI SISI BINADAMU TU WASAHAULIFU NA WALA HATUENDI KANISANI KUPEWA MATENDO MEMA KWANI KUTENDA MEAMA AU MABAYA NI UAMUZI WA MTU MWENYEWE  KADRI AKILI NA ROHO YAKE INAVYOMTUMA
...........>>>>BASI LEO TUTAFAKARI HAYA NA DAIMA TUWE WATU KUTENDA MEMA NA SI KWENDA KANISANI KILA JUMAPILI NA MSIKITINI KILA IJUMAA KWA LENGO LA KUJIONESHA KWA WATU KUMBE AKILI NA ROHO ZETU HUTUTUMA KUTENDA MABAYA
>>>>>>>>>>>MBARIKIWE NYOTE MNAOTAMBUA KUWA KUWA MCHA MUNGU NI "MATENDO NA SI MANENO,MICHANGO KANISANI AU MSIKITINI,KUTOA MSAADA KWA KUWA UNA UWEZO NA KADHALIKA.!
                                             <<<<<<>>>>
................................Na Mwalimu Mzoefu Darasani..........................
 Mwl.Mzoefu Darasani na Ubavu wake!!!                                                         Na Obama na Ubavu wake!
                                                                                                                   

Saturday, September 20, 2014

TUJIULIZE KWA NINI TUNAFANYA KAZI KUTWA KUCHWA!

                        MI IMANI YANGU :
   NI KWA SABABU KAMA BABA AU MAMA TUNAWAJIBIKA KWA FAMILIA ZETU,HIVYO PILIKA ZOTE HIZI ZA KUSAKA PESA,MALI,UWEZO,VYEO,NYUMBA,MASHAMBA,ELIMU,AFYA,MAZINGIRA BORA,BIASHARA NA MENGINE MENGI YANAYOFANANA NA HAYO NI KWA SABABU YA KUZIJENGEA MAISHA BORA FAMILIA ZETU.
  BASI TUFANYE KAZI ZETU KWA MOYO,UADILIFU NA KWA KUMCHA MUNGU ILI TUWEZE KUFANIKIWA,KWANI KILA JAMBO UNALOFAMYA UKIMSHIRIKISHA MUNGU UNAWEZA!!
>>>>>>>>Na Mwalimu Mzoefu Darasani>>>>>>>!!

Wednesday, September 17, 2014

JALI AFYA YAKO

 UMEFANYA MAZOEZI ANGALAU MEPESI YA VIUNGO?
         KAMA KAWAIDA YANGU KAMA "MWL.MZOEFU DARASANI"KUKUPATIA DONDOO ZA AFYA,ELIMU NA IMANI.LEO NITUMIE FURSA HII KUKUKUMBUSHA KUWA AFYA NDIYO MAMBO YOTE.
        UKIUGUA,BASI UTAMBUE KUWA HATA KAMA UTAMWONA DAKTARI NI LAZIMA ATAITAZAMA AFYA YAKO KWA MAMBO MATATU NAYO NI:-
1.CHAKULA UNACHOKULA
2.MAZOEZI KAMA UNAFANYA
3.DAWA ULIZOWAHI KUTUMIA
         HATIMAYE ATAPENDEKEZA UANZE NA KIPI, KUMBUKA TIBA YA KWANZA KWA AFYA YA MIILI YETU NI"CHAKULA" IKIFUATIWA NA MAZOEZI YA VIUNGO NA DAWA ZA HOSPITALI NA HATUA YA MWISHO. BASI TUNALOPASWA KULIFAHAAMU HAPA NI "LIFE STYLE" YETU KATIKA LISHE YA KILA SIKU NDIYO ITAKAYOTUTAMBULISHA MWENENDO MZIMA WA AFYA ZETU.
          KAMA MWALIMU MZOEFU DARASANI NASHAURI YAFUATAYO:-
  • Tujali kupata chakula kuliko kitu kingine chochote-tena milo mitatu.
  • Tuupangilie muda wetu kwa wiki kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu.
  • Tusiwe watu wa kukimbilia kutumia dawa hata kwa ugonjwa unaoweza kutoweka kwa kufanya tu mazoezi
  • Tusipendelee sana starehe zitutawale daima-tufanye kazi ni sehemu ya mazoezi.
  • Basi ukitaka mipango na maisha yako yote yaharibike, chezea afya kwa kutafuta magonjwa-"Bakia njia kuu"
<<<<<<<< Ni ushauri tu ....Na "Mwl Mzoefu Darasani">>>>>>>>

Monday, September 15, 2014

VIJANA WAKO NYUMBANI BAADA YA MITIHANI YAO YA TAR.10/9 HADI 11/9

          WATU WANASEMA "MUNGU NA MBIO"
   Tunashukuru mitihani imemalizika bila mizengwe,na sasa sisi kama wadau wa fani hii tunachokifanya ni kufanya maombezi yake kwa Mola ili watoto wetu waibuke na ushindi na kushinda mitihani hiyo na hatimaye kutimiza ndoto zao za kwenda sekondari-ndiyo malengo yetu sisi wadau na hasa "Mwalimu Mzoefu" Si unajua tena hii ndo fani aliyonipatia Mwenyezi Mungu lazima niitendee haki kwa wanadamu wanaonipatia watoto wao na kuniamini>>> Basi tuungane pamoja kuwaombea vijana wetu!!
!!!.................Na Mwalimu Mzoefu Darasani..............!!!  
 
 Walimu kazi yetu tumeifanya kwa moyo na uhodari mkubwa na sasa Baba wa wote ndiye mweny "maamuzi"....!!! 

Tuesday, September 9, 2014

MITIHANI - MITIHANI - MITIHANI -DRS VII HIYOOO!!

MIMI NISEME KAMA MWL MZOEFU DARASANI MAANDALIZI YALIKUWA MAZURI NA HASA KWA WANAFUNZI WA S/M MISUNKUMILO WILAYA YA MPANDA - MKOA WA KATAVI
            VIJANA WAPO TAYARI KWA MITIHANI HII NA NIMATUMAINI YANGU MAKUBWA WATOTO WATAFANYA VIZURI ,UKIZINGATIA NAMI NILIKUWA MIONGONI MWA TIMU ILIYOKUWA IKIWANOA WATOTO WA S/M MISUNGUMILO WALIOKUWEPO KAMBINI KWA TAKRIBANI SIKU 21
            WAKATI HUO HUO KAMBI YAO ILIFUNGWA RASMI NA AFISA ELIMU WA H/SHAURI YA MJI WA MPANDA BW, KAYOMBO KWA DUA, NASAHA, MAOMBI NA KUTOA MOTISHA KWA WANAFUNZI NA WALIMU WAO

Hapa chini wanafunzi wakiwa katika hekaheka za mwisho leo asubuhi shuleni Misunkumilo>>>>Tazama:>>








Saturday, July 19, 2014

UMEFIKA KATIKA KANISA HILI LA HIJA - HAPA MPANDA, KATAVI?

!!....Tembelea siku moja ufanye hija yako hapa kanisa la hija la Ilembo nje kidogo ya mji wa Mpanda.......!!

 !!Ni kanisa la hija lijulikanalo kama - Ilembo
    ~~~~Na Mwl.Mzoefu~~~~

                                                                              !!Wana-kwaya wa Parokia ya Ilembo!!
!! Wanatoka kanisani ibada imekwisha!!