Tuesday, November 24, 2015

MWALIMU MZOEFU DARASANI-LEO NA MITIHANI YA DARASA LA IV -KITAIFA;

UNAJUA NINI...AMBACHO HUKIJUI JUU YA MITIHANI YA DARASA LA IV!!
  • Wadau wanauandaa mtihani huu kwa mazoea tu kwa sababu bajeti yake ni ya kubabaisha na wakati mwingine shule zinalazimika kuchangia uendeshaji wake.
  • Wadau hawawaandai watahiniwa kama wale wa darasa la vii
  • Walimu wakuu unafika wakati wa kupambana na wazazi/walezi juu ya michango ya chakula kwa wanafunzi kwa siku mbili za mtihani-hii ni pamoja na kuwalipa wapishi
  • Watahiniwa hawaandaliwi kisaikolojia ikiwa ni pamoja kuwapatia viwango vya kitaifa vya ufaulu wa mitihani hii-hivyo mtahiniwa husalia gizani asielewe kuwa asipofanya nini kitatokea
  • Kutokana na uhafifu wa umuhimu wa mtihani huu-imefikia hata mzazi/mlezi hajawahi kushuhudia mtoto wake akikariri darasa kwa kushindwa mtihani huu na ndio maana hawajibiki ipasavyo kwa mtoto wake na wala shughuli zote zihusuzo mitihani hii kwa ujumla
  • Matokeo ya hayo yote-ni KUUONA MTIHANI HUU NI KAMA MILA NA DESTURI IKIFIKA MUDA WAKE BASI TUANDAE WATOTO WAKAFANYE....BASI!!
<><><><>Ni mtazamo wangu kama Mwl Mzoefu Darasani<><><><>!!!!!
NITUMIE NAFASI HII KUWATAKIA KILA LA KHERI WAANDAJI-WASIMAMIZI-NA WATAHINIWA WOTE-MTIHANI MWEEEEEMAAAAA!!!
<><><>Na MMD-S/M-M/MILO<><><>!!


 








Mwl Mzoefu Darasani(MMD)

Tuesday, November 17, 2015

LEO NA MWL MZOEFU DARASANI(MMD)....!!

NGOJA........NIZUNGUMZIE HII MITIHANI YA DARASA LA NNE KITAIFA TUNAYOIENDESHA NA KUISIMAMIA KILA MWAKA.
.......>>NIZUNGUMZIE UBORA WAKE NA UMUHIMU WAKE:
1.Umepungua kwa kiasi kikubwa:
  • Fedha za kuendeshea zinapunguzwa siku baada ya siku ..na huko tunakokwenda utatokea kuanza kuwachangisha wazazi
2.Hauna kiwango maalum cha ufaulu ..matokeo yake kila mwalimu mkuu anakiwango chake cha kuwapeleka watoto hao darasa la tano:
  • Kwa ujumla watoto hao wafaulu wasifaulu wanaingia darasa kama kawaida wala hakuna mdau yeyote anayeshituka na kukumbuka kuwa malengo ya mtihani huu ni kuwapima watoto na kuwachuja ili darasa la tano waingie kwa kichwa na si kwa miguu(waingie wenye uwezo tu)
  • Hakuna inayofuatilia wanafunzi walioingia darasa la tano baada ya mtihani...si wadau wa mkoa,wilaya wala kata- kazi inasalia kwa m/mkuu peke yake
3.Swali hapa na hoja kuu ni nani awajibike:
  • Wizara-haiupatii mtihani huu umuhimu unaostahili?
  • Maafisa elimu mikoa -  hawaoni umuhimu wake lakini wanaona fedha toka wizarani hivyo wazifanyie kazi zisirudishwe?
  • Maafisa elimu wilaya - wanapokea maagizo tu basi?
  • Waratibu elimu kata - wamezoea kuona mitihani hii ikifanyika kila mwaka na hivyo hawana haja ya kuuliza kama wanachokisimamia ni sahihi au la!?
  • Walimu wangu wakuu - wenye kupokea kama yalivyo hata kama hayajaiva...wanauzoefu wa kuyarudisha katika jiko mpaka yaive na kuliwa na wanafunzi wao?
MPAKA HAPO SINA MAELEZO MAZURI ZAIDI KAMA MWL MZOEFU DARASANI! ..NINACHOSHAURI KWA UZOEFU WANGU NI KWAMBA TUSIMAMIE MITIHANI YA SHULE VIZURI TU INATOSHA MBONA ENZI ZETU TULIKUWA TUKIFANYA VIZURI PASIPO MITIHANI HII?>>>>>>>>SIJUI WEWE UNA MAONI GANI YENYE MSAADA ZAIDI ....Toa maoni yako>>>...!!
              <<<<<
Darasa>>


 Boss wa elimu
<<                           















                                      MMD - Kulia>

Thursday, September 24, 2015

TUSHEREHEKEE IDD KWA KUPEANA ELIMU YA KUITUNZA AMANI TULIYONAYO....UKIZINGATIA!!!!! U-C-H-A-G-U-Z-I- NDO HUOOOOOO!!

NGUDU ZANGU WAISLAMU WAKATI TUNAKULA MAPOCHOPOCHO YETU TUKUMBUKE AMANI NI ZAIDI YA KUISHI HAPA TANZANIA

Nimesikia sasa hata kuwekeza sasa kigezo kimojawapo cha wawekezaji kuja kuwekeza,kwanza wanataka kuhakikishiwa usalama na amani juu yao>>>>> Lakini ni kweli kama kuna vurugu utafanya  kitu kweli!! SINA IMANI!!
                                          ~~~~~~~~~~~~!!Na Mwl Mzoefu Darasani~~~~~~~~~~~!!

a-m-a-n-i-a-m-a-n-i-a-m-a-n-i-a-m-a-n-i!!!

Thursday, September 10, 2015

MIAKA SABA(7) LEO-----BASI!!

SAA SITA NA NUSU MITIHANI INAKAMILIKA NA WATOTO WETU WATARUDI NYUMBANI KWA MAPUMZIKO MAFUPI KABLA YA KUINGIA SEKONDARI JANUARI 2016>>>NAWATAKIA KILA KHERI!!!!
                                                    >>><Na MMD>>><<<!!<<
                     MMD na MWL ANAYECHIPUKIA -KUFUATA NYAYO ZA MMD

Wednesday, September 9, 2015

MITIHANI YA DARASA LA SABA(VII) - NA MWL. MZOEFU DARASANI-TOKA MANISIPAA MPANDA,KATAVI

<<<<
>>>>>LEO NGOJA TUITUE NANGA MELI HII KATIKA BANDARI SALAMA-.LA MSINGI HAPA NI LIPI? TUNAAMINI WALIMU WENZANGU WAKISHIRIKIANA NAMI (MMD) KAZI YA KUWAANDAA ILIKUWA PEVU NA MAKINI 
>>>>>NI IMANI YETU NA MATOKEO NAYO YATATOKA KULINGANA NA TULIVYOWAANDAA VIJANA WETU----"MUNGU MBELE'---MBIO NYUMA"
>>>>>WANASEMA HIVI WASWAHILI----"USIJISIFU KUWA UNA MBIO BALI MSIFU ALIYEKUKIMBIZA" NAMAANISHA KUWA YOTE TULIYOYAFANYA SI UWEZO WETU BALI NI MUNGU ALIYESABABISHA
>>>>>BASI NAWATAKIA VIJANA WANGU WOTE TANZANIA NZIMA TUKUTANE SEKONDARI 2016
                                           ~~~~~~~Na Mwl Mzoefu Darasani~~~~~!!

Sunday, September 6, 2015

MIKAKATI YA KUIBUKA TENA NAFASI YA KWANZA MTIHANI WA VII 2015 MPANDA MANISPAA HII HAPA:

  1. KUJIAMINI
  2. KUKARIRI MAJIBU SAHIHI
  3. KUJAZA MASWALI YOTE
  4. KUFANYA MTIHANI KAMA KUFANYA ZOEZI TU
  5. KUTOULIZANA NINI ULIJIBU BAADA YA KILA MTIHANI KUMALIZIKA
N/B:- USHINDI NI MBELE KWA MBELEEEEE KAMA RANGI YA KUJANI NA NJANO!!
                     ...Na Mwalimu Mzoefu Darasani....!!

MITIHANI VII NI JUMATANO IJAYO - MPANDA MANISPAA KAZI KWENU KUTETEA USHINDI WA 2014

Wakati Jumatano 09/09/15 mitihani ikianza kwa dasara vii Manispaa ya Mpanda ina kibarua kizito cha kutetea nafasi walioipata mwaka jana kwa kunyakua nafasi ya kwanza kwa Halmashauri zote za miji Tanzania...Sasa mwaka huu  kunani? ...Lakini ngoja niwaulize kwani ninyi mmejipangaje? Kama Mna "buku" mmekwisha!! Fununu tu ---nasikia ushindi ni mbele kwa mbele kama wana-checheme!!!
                                              ~~~~~Na Mwl Mzoefu Darasani~~~~~!!

Thursday, September 3, 2015

MWALIMU MZOEFU DARASANI NA SIASA

IJAPOKUWA SIASA NI SEHEMU YA MAISHA,BADO KILA MMOJA ANA MAISHA BINAFSI NA FAMILIA YAKE - HUU NDIO UKWELI, BASI WAKATI UNAKWENDA KUCHAGUA  MWAKA HUU, ZINGATIA YAFUATAYO:-
  1. JIULIZE ALIYEKUFIKISHA HAPO ULIPO ALIFANYA LOLOTE AU SI CHOCHOTE
  2. WEWE ULITOA MCHANGO WOWOTE KATIKA KUFIKIA HAPO ULIPO
  3. JIULIZE KAMA AMANI ILITOA MCHANGO FULANI KATIKA KUFIKIA HATUA ULIONAYO
  4. JIULIZE PIA WEWE MWENYEWE ,JE, UNAPENDA AMANI ITAWALE?
MMD (Mwl Mzoefu Darasani) NASEMA HIVIII....CHAGUA "AMANI" UTAONA KILA KITU KITAWEZEKANA!!!

Saturday, August 22, 2015

HARAKATI ZA KUTETEA USHINDI WA KWANZA KITAALUMA-KWA HALMASHAURI ZOTE TANZANIA

ILI KULINDA NAFASI YA KWANZA LAZIMA JASHO LIKUTOKE MARA MBILI ZAIDI!!!!!
HALI HII INAJITOKEZA KWA SASA KWA MANISPAA YA MPANDA MKOA WA KATAVI.KWA KWELI WALIMU WAKO "BUSY" KUHAKIKISHA WANATETEA TENA UBINGWA WALIOUNYAKUA MWAKA JANA 2014 KWA KUWA HALMASHAURI YA KWANZA NCHINI KWA MATOKEO YA DARASA LA VII 2014
      LAKINI SIO SIRI KAZI IPO-WASWAHILI WALISEMA "MTAFUTA CHA UVUNGUNI SHARTI AINAME" NA KWELI TUNAINAMA KIKWELI-KWELI!!
~~~~~~~~~~~Na Mwl.Mzoefu Darasani~~~~~~~~~~!!

Tuesday, June 23, 2015

WATANGAZA NIA

UKITAKA KUFAHAMU VIONGOZI WALIO WENGI WANAJUA PESA ZA WATANZANIA ZINAKOCHOTWA BASI ANGALIA WENGI WALIVYOTANGAZA NIA
>>>>>>>Na Mwalimu Mzoefu Darasani>>>>>>
Tumia mamilioni katika NIA upate mabiloni kwa watanzania wenzako!!

Saturday, May 16, 2015

KARIBU-TUJUMUIKE NA MWALIMU MZOEFU DARASANI-TUPATE MA-TAALUMA YANAVYOENDELEA HAPA NYUMBANI TANZANIA

HEBU LEO TUANZE NA HILI LINALOFUKUTA KWA SASA JUU YA ELIMU YA SEKONDARI KUUNGANISHWA NA SHULE YA MSINGI-SEHEMU-1
>>>>>SERIKALI IMEAMUA KUANZISHA MPANGO HUO BILA KUFAFANUA MANUFAA YAKE. SWALI HAPA NI KWAMBA,JE,WADAU WOTE WAMESHIRIKISHWA NA KUNA MAANDALIZI YA KIASI GANI ILI WADAU HAWA WAWEZE KUHAMIA HUKO SERIKALI INAKOTAKA?
>>>>>>MWALIMU MZOEFU ANASEMAJE KWA HILI?
Ukitaka kuthubutu jambo lolote lie liwe la kibiashara, kilimo, ufugaji,kiofisi au kielimu kama hili,washirikishe wenzako,upate mawazo yao,uzoefu wao,utaalamu wao kisha,kusanya mambo hayo kaa na mwenzako yachuje na mwishi utaibuka na kitu safi (pure) kwani faida na hasara utakuwa unaifahamu lakini kwa hili sijui>>>>tuwe pamoja sehemu ya pili
                                                      ~~~Na Mwl Mzoefu Darasani!!!

Thursday, January 1, 2015

MWAKA MPYA NA "MWALIMU MZOEFU DARASANI"

KWANZA TUMSHUKURU MUNGU KWA KUKUBALI KUTUACHIA VIBALI VYA KUENDELEA KUISHI,INGAWA TUNAELEWA FIKA VIBALI HIVYO VILIVYOCHAFUKA KWA MADHAMBI YA MWAKA MZIMA:


>>>Hebu tuchukue yale mazuri ya mwaka jana tuyaendeleze na kuyatenda mwaka huu,aidha mipango - mikakati ambayo hatukufikia malengo mwaka jana,tumwombe Mungu atunyooshee mkono wake wa baraka tuyakamilishe mwaka huu, na bila kusahau kuweka mpango-mkakati wa mwaka huu tena....Basi Mungu ndo mambo yote na ndo aliye 'busy' peke yake huko mbinguni na hapa duniani binadamu tunajidanganya tu tunaposema tupo busy!!
<<<<<Na:- Mwl.Mzoefu Darasani<<<<<
Mr & Mrs Haule(MMD)